Tuesday, January 31, 2012

SAMWEL DANIEL NA KAINDI TARATIBU WAKIMEREMETA…!

Wakiwa na nyuso za furaha bwana harusi Samwel  Daniel  na mkewe Kaindi  Taratibu wakiwa kwenye pozi la  picha baada ya kufunga ndoa yao katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Kibaha hivi karibuni na kufuatiwa na sherehe kubwa iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi   Luxiry jijini Dar es Salaam.

 Makaka wa bwana harusi wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa sherehe ya harusi ya mdogo wao .
Bw. Harusi akipita juu ya migongo ya wazazi wake wakati wa kuingia ukumbini wakati wa harusi yake iliyofanyika katika ukumbi wa Mbezi Luxiry jijini ,Dar es Salaam,utamaduni huu hufanywa na watu wa Lindi kabila la wayao.
Bibi Harusi akipita juu ya migongo ya wakwe zake wakati wa kuingia ukumbini ikiwa ni ishara ya kukaribishwa katika familia, kabila la Wayao .
Bw.harusi  Samwel akiwa na mkewe Kaindi wakishuka kutoka katika mlima kilimanjaro  uliopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, walipokwenda kufanya utalii wa ndani.Baada  ya kufunga ndoa yao kwa Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Januari 28, 2012.

No comments:

Post a Comment