Familia ya marehemu John Franklin Chekani wa Mzumbe- Morogoro, wanatoa shukrani zao za dhati kwa madaktari na manesi wote wa Hospitali ya AghaKhan -Dsm Tanzania na Hospitali ya Roman Catholic ya Windhoek-Namibia, waliojaribu bila kuchoka kuokoa maisha ya mpendwa wetu.
Pia tunamshukuru Katibu Mkuu na wafanyakazi wote wa TAMISEMI, Mkurugenzi na wafanyakazi wote wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF) Tanzania, Mkuu wa chuo, mlezi, wafanyakazi na wanafunzi wa chuo cha Polytechnic, Mch. Noleen West na washarika wote wa kanisa la mtakatifu George, familia za Bw. Tomeka, Bw. Mahindi, Mwenyekiti,na wanajumuiya wote wa Tanzania wanaoishi Namibia waliojitokeza kwa moyo mmoja.
Shukrani za dhati pia ziwaendee Mrs. Jane Fatukubonye, Mariam Mbegu,na wanajamii wa Mkongeni na Mzumbe kwa juhudi za uwezeshaji wa msiba huo. Pia tunazishukuru kwaya zote zilizoshiriki, kwaya ya mzumbe, ya Dodoma na kwaya ya kibaha na wachungaji wote walioshiriki katika msiba.Pia tunawashukuru wote ambao kwa namna moja au nyingine wamewezesha kutufariji katika kipindi hiki kigumu cha kufiwa na mume , baba na babu yetu mpendwa MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI. AMINA

No comments:
Post a Comment