Monday, January 30, 2012

AIRTEL YAKABIDHI GARI LENYE THAMANI YA TSHS MILIONI 35 RUKWA

Hatimae  Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imekabidhi gari lenye thamani ya shilingi milioni sitini na tano kwa mshindi wa shindano la Jivunie lililofanyika 2010 bwana Immanuel Kapungu mkazi wa Sumbawanga katika kijiji cha Muze.

Akikabidhi zawadi hiyo kwa mshindi  huyo mkuu wa wilaya  ya Sumbawanga Kanali mstaafu John Mzurikwao amesema kutolewa kwa gari hilo ni changamoto kwa wateja wengine  kushiriki mashindano.

Gari hiyo aina ya Toyota Rav 4 inakuwa ni gari ya pili kutolewa mkoani Rukwa huku mshindi mwingine akiwa amekwisha kabidhiwa mwezi wa nane mwaka jana kama  anvyoeleza meneja wa biashara wa AIRTEL kanda ya nyanda za juu kusini Fredrick Mwakitwange.
na kajunasu blog

No comments:

Post a Comment