Monday, January 30, 2012

KUMEKUCHA TAMASHA LA PASAKA

NA SAMIA MUSSA
BAADA ya kuwasilisha ripoti ya tamasha lililopita kwenye Baraza la sanaa la taifa (BASATA), Kampuni ya Msama Promotions, imeanza rasmi maandalizi ya tamasha la mwaka huu.
Hatua za awali za maandalizi hayo ni pamoja na kuomba vibali katika baraza hilo vya kufanyika kwa tamasha hilo ambalo hufanyika kila mwaka, likiwa na lengo la kusaidia jamii.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa mjadala wa upataji wa kibali hicho uliofanyika kwenye ukumbi wa BASATA, mjumbe wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo Jimmy Rwehumbiza , alisema kuwa wapo katika hatua za mwisho za kupata kibali.
Naye mratibu wa tamasha hilo kwa upande wa BASATA, Malimi Mashiri ‘Ngosha’ alisema kuwa pamoja na kuwa wazoefu wa kufanya matamasha hayo kuna umuhimu wa mwakilishi kutoka katika baraza hilo.
“Kuna umuhimu wa mwakalishi wa BASATA, kuwepo katika matasha yote ili kujua kinachofanyika ikiwa pamoja na ugawaji wa misaada kwa walengwa,” alisema Ngosha.
Aidha, Ngosha alisema kuwa kuwepo kwa mwakilishi wa BASATA, kutaisaidia kampuni hiyo kufanya matamasha mengine kiurahisi kwa kuwa inaweza ikarahisishiwa mambo mbalimbali katika baraza hilo.
Kampuni hiyo imekuwa ikifanya matamasha kila mwaka yakiwa na lengo la kuisaidia jamii ambapo kwa mwaka huu itatoa mitaji kwa wajane wasiopungua 100, Baiskeli 150 za walemavu, ambapo idadi ya kusomesha watoto yatima imeongezeka kama kwa wajane 50 hadi 100.

No comments:

Post a Comment