Mwenyekiti ya Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii,ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Peramiho,Mh Jenista Mhagama akizungumza jambo mbele ya kamati hiyo (haipo pichani) pamoja na uongozi wa Clouds Media Group mapema jana,Mikocheni jijini Dar,ambapo kamati hiyo imefanya ziara ndani ya kampuni hiyo na kujionea mambo mbalimbali yanayofanywa na kampuni hiyo.Aidha Mh Mhagama ameisifu na kuipongeza kwa kiasi kikubwa kampuni hiyo kwa utendaji wao mzuri wa kazi na pia kaitoa nafasi kubwa ya ajira kwa vijana.
Mmoja wa mainjinia wa Clouds TV,Mebb Hadhad akifafanua jambo kuhusiana na urushaji wa matangazo ya TV mbele ya kamati hiyo ambayo haipo pichani.
Mmoja wa wakurugenzi wa Clouds Media Group,Ruge Mutahaba akielezea jambo mbele ya kamati ya bunge ya Maendeleo ya jamii kuhusiana na utendaji kazi wa kituo cha Clouds TV na mambo mbalimbali yahusuyo mfumo wa masafa ya digitali ambayo kituo hicho inatarajia kujiunga nayo.
Mh Jenista Mhagama akizungumza jambo ndani ya studio za clouds fm akiwa sambamba na kamati yake huku kipindi cha Leo Tena kikeendelea.
No comments:
Post a Comment