Waziri Mkuu Mizengo Pinda
---
Madaktari walijumuika ukumbi wa CPL leo asubuhi kusubiri ujio wa PM.ambae meshafika na maongezi yameanza.Dk.Ulimboka yuko mbele na madaktari bingwa wako mbele.tutawajuza zaidi
--
Katibu mkuu na mganga wa serikali wameondolewa, waziri na naibu waziri watashughulikiwa na rais, call allowances za madaktari bingwa ni 25000/= na madaktari wa kawaida ni 20000/=,madaktari watapewa nyumba na green card..
Madaktari wamekubali offers za serikali na wametoa mwezi mmoja kuona kama kweli serikali inatekeleza kwa dhati ahadi zake.Kesho wataingia kazini .kikao kinaendelea
*Taarifa ya Ofisi yaWaziri Mkuu Juu ya Kikao Cha Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Madakatari ipo hapo chini
--
WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA YUPO DAR ES SALAAM KUTOKA DODOMA KUSHUGHULIKIA MGOMO WA MADAKTARI AMBAO UMEKUWA UKIENDELEA KWA LENGO LA KUUPATIA UFUMBUZI.LEO AMEKUTANA NA UONGOZI WA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI PAMOJA NA MADAKTARI BINGWA KUTOKA SEKTA YA UMMA NA BINAFSI NA WASTAAFU.
KESHO(LEO) SAA 3 ASUBUHI ATAKUTANA NA MADAKTARI BINGWA, MADAKTARI WALIOSAJILIWA (REGISTRALS) NA MADAKTARI WALIOKO KWENYE MAFUNZO KWA VITENDO (INTERNS) NA BAADA YA HAPO SAA 4 ATAKUTANA NA WAFANYAKAZI WA HOSPITALI YA MUHIMBILI, MOI, OCEAN ROAD NA WAWAKILISHI KUTOKA HOSPITALI ZA MKOA WA DAR ES SALAAM, KWENYE UKUMBI WA CPL, MUHIMBILI.
MATARAJIO YA SERIKALI NI KWAMBA MAZUNGUMZO HAYO YATAWEZA KUMALIZAMGOGORO HUU NA MADAKTARI WOTE KUREJEA KAZINI NA HIVYO KUREJESHA HUDUMA ZA MATIBABU KATIKA HALI YA KAWAIDA KWA WANANCHI WA TANZANIA.HIVYO SERIKALI INAWAOMBA WOTE WANAOHUSIKA WAFIKE KATIKA MIKUTANO HIYO BILA YA KUKOSA.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU






No comments:
Post a Comment