Wednesday, March 28, 2012

Royal bakery ya jkt kawe yavamiwa na majambazi usiku huu,wakomba fedha za mauzo na kuwalaza chini wafanyakazi.


Masikini Dada wa watu akilia kwa uchungu,huku polisi wakiendelea kuchukua maelezo.





Baadhi ya wafanyakazi wa Bakery hiyo wakiwa wameduwaa wasijue la kufanya kwa muda huo mara baada ya majambazi kupora kiasi cha fedha ambazo haikuweza kubainika mara moja ni kiasi gani mpaka Camera ya Jiachie inaondoka eneo la tukio usiku huu.


********
Kwa mujibu wa mmoja wa wafanyakazi wa Royal Bakery hiyo ameeleza kuwa tukio la kuvamiwa na majambazi eneo hilo imetokea mnamo majira ya saa 3 na ushehee hivi (usiku huu),anasema majambazi hao walikuwa watano waliwasili eneo hilo wakiwa na piki piki mbili na gari. Mmoja aliyekuwa ameshika bastola aliingia ndani na kuwaamuru wafanyakazi waliokuwemo ndani wote walale chini,na kuanza kuchukua fedha za mauzo zilizokuwemo kwenye droo zao za kuhifadhia fedha,huku wengine nje wakifyatua risasi hewani na kufunga barabara kwa muda wa dk 10 hivi.

Dada huyo aliyejikuta akiangua kilio wakati akielezea,anasema kuwa yeye amepigwa pigwa makofi na hakujeruhiwa,kama vile haitoshi anasema kuwa eneo hilo pia kulikuwepo na wazungu wapatao watatu ambao walienda pale kujipatia huduma mbalimbali,kwa bahati mbaya wakakutana  na dhahma hiyo,ambapo nao walilazwa chini na kuporwa wallet zao sambamba na pete zao walizokuwa wamevaa mikononi,baada ya ambush hiyo majambazi wakatoweka kusikojulikana ndipo difenda ya polisi ikawasili na kuanza kuchukua maelezo kadhaa
Picha na habari kwa hisani ya Jiachie Blog

No comments:

Post a Comment