Thursday, April 26, 2012

BENKI YA NBC YAANDAA MKUTANO WA MASUALA YA KIUCHUMI

Maofisa wa ABSA Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya
Afrika Kusini wakiwa katika  mkutano wa masuala ya kiuchumi
ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital jijini Dar es Salaam jana
jioni. Katikati ni Ridle Markus, Jeff Gable (kushoto), Pius Tibarazwa
(wa pili kushoto) wa NBC Tanzania na Michael Keenan (kulia) wa ABSA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Lawrence Mafuru
(kushoto) akimsikiliza mmoja wa maofisa wa  ABSA Capital ambayo ni
sehemu ya benki ya ABSA ya Afrika Kusini, Jeff Gable,  katika mkutano
wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA Capital kwa
wateja wa makampuni wa NBC, jijini Dar es Salaam jana jioni. Wa pili
kushoto ni Mohamed Sayed wa ABSA Capital na Mkuu wa Idara ya Fedha na
Masoko wa NBC, Pius Tibarazwa
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Lawrence Mafuru (katikati)
akisalimiana na baadhi ya wateja wa makampuni wa benki hiyo katika
mkutano wa masuala ya kiuchumi ulioandaliwa na NBC pamoja na ABSA
Capital ambayo ni sehemu ya Benki ya ABSA ya Afrika Kusini jijini Dar
es Salaam jana jioni.

No comments:

Post a Comment