Mabingwa wa soka 2012/2013 timu ya Uhasibu tawi la Singida -Uhasibu imeibuka bingwa, baada ya kushinda kwenye mashindano ya tamasha la michezo lilioandaliwa na CRDB benki kupitia akaunti yake ya ‘Scholar’.
Afisa wa CRDB benki tawi la Singida mjini William akizungumza muda mfupi kabla ya kufungwa kwa tamasha la michezo lililoshirikisha vyuo vya Uhasibu, Uhazili, VETA na chuo cha Ualimu cha mjini Singida.
Kaimu Mkuregenzi wa manispaa ya Singida ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga tamasha la michezo kwa vyuo mbalimbali vilivyopo mjini Singida Simon Hoja, akizungumza kwenye kilele cha tamasha hilo. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Na Nathaniel Limu.
Timu ya soka ya chuo cha Uhasibu (TIA) tawi la Singida imetawazwa mabigwa wa tamasha la michezo la CRDB benki akaunti ya ‘scholar’ kwa mwaka wa 2012/2013, baada ya kuichapa timu ya uhazili magoli 2-1.
Mchezo huo wa fainali ambao ulikuwa mkali na wa kusisimua, ulifanyika kwenye uwanja wa Namfua mjini Singida na kwa ushindi huo, Uhasibu imezawadiwa mabeberu matatu makubwa ya mbuzi.
Uhasibu ilionyesha mapema dhamira yake ya kuibuka na ushindi kwenye mechi hiyo, baada ya Kalisti kipalazya, kuipatia timu hiyo goli la kwanza katika dakika ya sita.
Kalisti ambaye aling’ara kwenye mchezo huo, alifunga goli hilo baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Samson Mwaipungu na kuachia shuti kali lililoenda moja kwa moja ndani ya lango la Uhazili upande wa kulia, huku kipa wa Uhazili Yohana Jumanne akilamba vumbi upande wa kushoto.
No comments:
Post a Comment