Wote kama wadau wa tasnia ya filamu na habari tumehuzunika kwa kuwa hatukutegemea kutokea yaliyotokea.
Lakini kifo cha ndugu yetu na mpendwa wetu ndio kiwe kiuzio cha magazeti..? Kila kukicha mara hivi mara vile huku mkijua kabisa mnachokiandika ni ‘Fix’ ili gazeti liuze. Au ndio kutimiza msemo usemao “Kufa Kufaana”..?
Wadau wana MO BLOG tunauliza. Kisingetokea kifo hicho ina maana magazeti yangekuwa ‘Empty”…??
Sisi wana MO BLOG hatudhani kama ni uungwana kugeuza msiba wa mwenzetu kuwa ‘dili’ ya kuuza magazeti yapo mengi yanayotokea katika jamii yetu ambayo tunapaswa kuwahabarisha wasomaji wetu AU?
Mimi Lemmy Hipolite wa MO BLOG naomba kutoa hoja binafsi na kuiwasilisha kwenu wadau kama nimepotoka nirudisheni kwenye barabara………!!!!
source.moe blog
No comments:
Post a Comment