Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando (kulia) akitangaza kuongezeka kwa zawadi ya hadi Tsh 143 m/-katika promosheni ya Nani Mkali itakayoendelea kwa muda wa miezi miwili zaidi, kushoto ni Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Dangio Kaniki akifuatilia wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani). Ili kushiriki promosheni andika neno “Mkali” tuma kwenda 15656 bure. Baada ya hapo utatumiwa maswali na kila utakapotoa jibu sahihi utapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10. Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shilingi 350 pamoja na kodi.
Afisa Uhusiano wa Airtel, Bi Dangio Kaniki (kushoto) akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa habari (hawapo pichani) jinsi ya kushiriki promosheni ya Nani Mkali iliyoongezwa muda. Andika neno “Mkali” tuma kwenda 15656 bure. Baada ya hapo utatumiwa maswali na kila utakapotoa jibu sahihi utapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10. Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shilingi 350 pamoja na kodi. Kulia ni Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mmbando.
----
-Promosheni ya Nani Mkali kuendedelea kwa miezi miwili
Mei 30, 2012.
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeongeza muda kwa wateja wake kuendelea kucheza promosheni yake kabambe ya Nani Mkali ambayo ilianza miezi mitatu iliyopita na kuwafaidisha zaidi ya wateja 90 wa Airtel waliojishindia jumla ya milioni 217 kwa mgawanyo wa kuanzia milioni 1 kila siku, milioni 3 kila wiki na milioni 30 kwa washindi wa mwezi.
Akiongea na waandishi wa habari leo Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema promosheni hii imekuwa na faida kwetu Airtel wateja wetu waliokuwa wakishiriki wameifurahia na ndio maana leo tumeamua kuongeza zawadi na muda wa promosheni ya Nani Mkali
Hivyo promosheni yetu inaongezwa muda wa miezi miwili huku zawadi zitakazo toka ni pesa taslim Jumla ya ya shilingi milioni 143 katika mgawanyo wa kuanzia shilingi milioni 1 kila siku-washindi 52, milioni 3 kila wiki –washindi 7,na milioni 30 kwa kila mwezi itatoka kwa washindi 2.
Pia tutakuwa na washindi wengine watakaogawana kitita cha shilingi milioni 10 za zaidi ikiwa watakuwa kati ya wachezaji bora wa promosheni ya Nani mkali
Ili mteja kushiriki na kujishindia zawadi hizi kabambe Afisa Mawasiliano wa Airtel bi Dangio Kaniki alisema,” kudhihirisha kauli mbiu yetu ya jisikie huru katika promosheni hii mteja anatakiwa kuandika neno “Mkali” na kutuma kwenye namba 15656 bure kabisa ili kujiunga. Baada ya hapo atatumiwa maswali na kila atakapo toa jibu sahihi atapata pointi 20 na jibu lisilo sahihi pointi 10.Kila ujumbe wenye jibu utatozwa shillingi 350 pamoja na kodi.
Promosheni hii pia itatoa fursa kwa wateja kuchagua lugha wanayotaka kwa kutuma neno “swa” kwa Kiswahili au “eng” kwa lugha ya kiingereza kwenda namba 15595 Kujua alama ulizonazo au point mteja wetu atatakia kutuma neno “point” au “alama” kupatiwa pointi alizojikusanyia. Kujiondoa kwenye promosheni mteja atatakiwa kutuma neno “cancel’ au “stop” kwenda namba 15595
Promosheni ya nani mkali ilizinduliwa rasmi februari 15, 2012 na kudumu kwa muda wa miezi mitatu.Nani Mkali imefanikiwa kuwazawadia wateja wa Airtel kutoa mikoa mbali mbali ikiwemo Arusha, Muheza Tanga and DSM, Tabora, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Kilimanjaroa na mingine mingi.
No comments:
Post a Comment