Sunday, May 13, 2012

Matokeo ya Timu ya Tanzania DMV Watoka bila kufungana na timu ya Ethiopia ya Maryland U.S



Mdhamini mpya wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya (Kwetu Fashion Design) Missy Tetemeke akiwa kwenye mpango mzima wa kuangalia na kuiunga mkono Timu ya Watanzania DMV, (Picha ya Kulia) Dogo Hudhaifa Shatry akisikiliza kelele za mashabiki wa timu hiyo.

Kikosi kamili cha timu ya waTanzania DMV wakiwa na mdhamini mpya wa timu hiyo Mbunifu wa mitindo ya Kwetu Missy Temeke, akiwana na shabiki Didi Vava, katika uwanja wa Greencastle, uliopo Burtonsville, Maryland

Tanzania DMV leo hii  iliweza kutinga tena uwanjani kucheza mchezo wake wapili na timu ya Ethiopia, hadi mpira kumalizika timu hizo zimetoma 0-0 katika  mpango mzima wa ligi ya 2011 Diaspora World Cup zinazoendelea katika viwanja vya Hyattsville na Germantown jijini Maryland Nchini Marekani



Mdhamini wa timu ya waTanzania DMV ambae ni mwana mitindo na mbunifu wa mitindo ya Kwetu Fashion Design, Missy Tetemeke akiwa na Bendera ya Taifa.
Mchezaji wa timu ya Ethiopian akipambana vikali na Yousouf Godson Liuzinho, kipindi cha kwanza katika ligi ya 2011 Diaspora World Cupkwenye kiwanja cha  Greencastle, kiliopo Burtonsville, Maryland.
Benchi la timu ya waEthiopia wakiwa kama mtu nane njee na ndicho kilicho wasaidia kutoka bila kufungana na Timu ya waTanzania DMV.  
Wachezaji wa wa timu ya Ethiopia wakiwania Freekick katika dakika ya 62 ya mchezo huo

No comments:

Post a Comment