Tuesday, May 29, 2012

MH. KAGASHEKI AWASIMAMISHA VIGOGO WANNE TANAPA KUFUATIA FARU WAWILI KUUAWA HIFADHI ZA SERENGETI.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki (kulia) akizungumza wakati akitoa tamko la kuwasimamisha kazi baadhi ya watumishi wa TANAPA ili kupisha uchunguzi dhidi ya mauaji ya Faru wawili. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wanyamapori Pauli Sarakikya.

Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Balozi Khamis Kagasheki amewasimamisha kazi vigogo wanne na watumishi kadhaa ili kupisha uchunguzi ufanyike kufuatia tukio la wanyapori wawili aina ya Faru kuuawa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti eneo la Moru.
Mh. Balozi Kagasheki amewataja vigogo hao kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi wa TANAPA Justin Mhando, Mkuu wa Kitengo cha Itelijensia wa TANAPA Emil Kisambo.
Wengine ni Mkuu wa Hifadhi ya Serengeti Mtango Mtaiko na Mratibu wa Mradi wa Faru Serengeti Nyafuru Nyamafumbati.
Pamoja na hao pia watumishi wengine28 wameandikiwa barua za kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tukio hilo.


No comments:

Post a Comment