Wednesday, May 30, 2012

MH. MAKALLA AIBARIKI TIMU YA TAIFA YA GOLF KWA KUIKABIDHI BENDERA KUELEKEA MASHINDANO YA CHALENJI YA AFRIKA.


Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi Bendera kwa Timu ya Taifa ya mchezo wa Golf inayotarajiwa kusafiri kwenda Gaborone Botwsana kushiriki katika mashindano ya chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Bw. Dioniz Malinzi na Kushoto ni Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Mh. Mary Chetanda.
Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mh. Amos Makalla (kulia) akipokea tiketi za wachezaji kutoka kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Precision Air Bw. Patrick Ndekana ambao ndio waliodhamini usafiri wa kwenda na kurudi pamoja vifaa vya Michezo vyenye thamani jumla ya zaidi ya Shilingi Milioni 7. Anayeshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Msafara wa timu hiyo Mh. Mary Chetanda (kushoto).



Pichani Juu na Chini Wachezaji wa Timu  ya Taifa ya mchezo wa Golf watakaoiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Chalenji ya Afrika kwa upande wa Wanawake yakayofanyika nchini Gaborone Botwsana.  Kutoka kushoto ni Madina Iddi, Ayne Magombe na Hawa Wanyeche katika pozi mbele ya Camera ya MO BLOG.

chanzo ,

No comments:

Post a Comment