Waziri wa Afrika Mashariki Mh. Samwel Sitta akisoma hotuba ya Rasimu ya Uzinduzi wa Kamati ya Kusimamia Utekelezaji wa Itifaki ya Soko la pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo amesema utekelezaji wa itifaki wa soko la pamoja hauendi kwa kasi iliyotarajiwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwa ni pampja na nchi wanachama kuchelewa kukamilisha zoezi la kuhuisha sheria zinazosimamia utekelezaji wa itifaki hiyo katika nchi zao.
Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Baraza la Mawaziri la Kisekta la Jumuiya la mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Afrika Mashariki na Mipango katika mkutano wao wa 15 uliofanyika Januari 2012 Kampala-Uganda liliziagiza nchi wanachama kuunda kamati za kitaifa za kitaifa za kusimamia Utekelezaji wa soko la pamoja. ( National Committee on Common Market Implementation Protocol).
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya Makatibu Wakuu na Wakuu wa Taasisi na Idara za Serikali.
No comments:
Post a Comment