Tuesday, May 29, 2012

MUSTAFA SABODO ATOA BILLIONI 5 KWA AJILI YA UJENZI WA JENGO LA KUEGESHA MAGARI JIJINI

Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa akimkabidhi Mfanyabiashara maarufu nchini, Mustafa Sabodovibali vya ujenzi wa jengo hilo, kushoto ni  Mwenyekiti wa Madhehebu  ya Khoja Shia Shiraz Walji
--
MFANYABIASHARA maarufu nchini, Mustafa Sabodo ametoa zaidi ya sh.bilioni 5 kwa madhehebu ya Khoja Shia Ithnaashri Jamat kwa ajili ya kujenga jengo la maegesho ya magari.
 
Akizungumza katika hafla ya kupokea vibali vya ujenzi wa jengo hilo Dar es Salaam leo kutoka kwa Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa alisema jengo hilo litasimamiwa na madhehebu hayo.
 
Alisema jengo hilo lililopo katika mitaa ya India na Morogoro la ghorofa 14 litakuwa na uwezo wa kuhifadhi magari 180 kwa wakati mmoja.
 
Silaa alisema fedha zitakazopatikana kwa malipo ya maegesho ya magari katika kipindi cha miaka 10 zitafanya kazi ya kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.Meya alisema kwa muda mrefu Jiji la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na maeneo ya kuegesha magari na kuwa jengo hilo la kwanza kubwa litakuwa ni mkombozi mkubwa.
 
"Kwa muda mrefu tumekuwa na matatizo ya kuegesha magari katika jiji letu hivyo msaada aliotoa ndugu yetu Sabodo kwa madhehebu hayo ya ujenzi wa maegesho hayo itasaidia sana kupunguza tatizo hilo," alisema Silaa.
 
Alisema Manispaa imepokea jambo hilo kwa mikono miwili na ndio maana imekamilisha vibali ili ujenzi huo uende pasipo kikwazo chochote.
 
Alisema jengo hilo litaitwa Sabodo Car Park jambo litakalo weka kumbukumbu ya mchango wake katika kufanikisha shughuliza za maendeleo.
 
Mwenyekiti wa Madhehebu hayo Shiraz Walji, alimshukuru Sabodo kwa msaada wake huo na kuahidi kusimamia vizuri mradi huo ambao utakuwa wa manufaa kwa Watanzania wote


No comments:

Post a Comment