Mashindano ya kuwania taji la Redds Miss Tanzania 2012 yanazidi kupamba moto kwa ngazi za vitongoji nchini kote huku vitongoji kadhaa vikiwa tayari vimesha fanya mashindano yake na vingine vikiendelea na maandalizi.
Wakati wiki hii Mashindano hayo yakitraji kufanyika katika Vitongoji vya Kurasini Jijini Dar es Salaam tayari Wanyange wanaowania taji la Redds Miss Cha'gombe 2012 nao wapo katika mazoezi tayari kwa fainali zao zitakazo fanyika mapema mwezi ujao.
Pichani ni warembo wa Chan'gombe wakiwa katika picha ya pamoja iliyopigwa muda mfupi baada ya kumaliza mazoezi yao Mei 22,2012 katika ukumbi wa TCC Chan'gombe jijini Dar es Salaam.
Warembo hao 11 wanataraji kupanda jukwaani mapema mwezi ujao kuwania taji hilo na kuwania tiketi ya kushiriki Miss Temeke 2012.
No comments:
Post a Comment