Tuesday, June 12, 2012

CHADEMAYATUMA RAMBIRAMBI KWA TAIFA LA KENYA, KUFATIA KIFO CHA WAZIRI SAITOTI.

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo kupitia Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imepokea kwa masikitiko ajali mbaya ya helkopta iliyokatisha uhai wa aliyekuwa Waziri wa Usalama wa Ndani wa Kenya, Profesa George Saitoti pamoja na Naibu wake, Orwa Ojode na maofisa wengine wa juu katika wizara hiyo.
Kurugenzi ya Mambo ya Nje ya CHADEMA inatumia fursa hii kutuma salaam za rambirambi na pole kwa Balozi wa Kenya nchini na kuwatakia moyo wa subira wananchi wote wa Kenya katika wakati huu wa majonzi ya kuondokewa na mmoja wa wanasiasa na kiongozi wao mwandamizi.
Hayati Saitoti, ambaye aliwahi kuwa Makamu wa Rais wa Kenya, akishikilia nafasi hiyo kwa muda wa miaka 13, pamoja na kuwa mmoja wa wanasiasa waandamizi nchini Kenya, atakumbukwa pia kama mmoja wa wanazuoni mahiri katika masuala ya uchumi, hesabu na mtunga sera.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, amina
Imetolewa leo Juni 11, 2012, Dar es Salaam na;
Ezekia Wenje (MB)
Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CHADEMA


No comments:

Post a Comment