PST inapenda kuujulisha umma wa watanzania kuwa inazindua Wiki ya Famasi ya Taifa “National Pharmacy Week (NPW)” ambayo itaadhimishwa nchi nzima.
Kutokana na ongezeko la mahitaji ya dawa, PST imeona kuwa ni vema kuhamasisha na kuelimisha umma kuhusu matumizi sahihi na utunzaji bora wa dawa nyumbani ili kuokoa maisha.
Katika wiki inayoanza 11 – 15 Juni mwaka huu PST imepanga kufanya shughuli mbalimbali katika jamii kikubwa ikiwa ni kutoa elimu kwa jamii.
Katika wiki hiyo kutakuwa na mahojiano ya papo kwa papo kwa wagonjwa na wananchi katika maeneo mbalimbali ambapo vipeperushi vilivyobeba ujumbe wa wiki vitagawiwa.
Vilevile ujumbe kwa wananchi utatolewa kwa kutumia vyombo vya habari ili elimu ya matumizi sahihi na utunzaji bora wa dawa majumbani uweze kuwafikia walio wengi.
No comments:
Post a Comment