Sunday, June 10, 2012

DKT. BILAL AFUNGUA MAONYESHO YA KWANZA YA TANZANIA HOMES EXPRO.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu ujenzi wa Nyumba za Shirika la nyumba la Taifa, NHC, kutoka kwa Ofisa Masoko wa Shirika hilo, Mariam Ndabagenda, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja Mauzo wa Shirika hilo, William Genya (wa pili kulia) ni Ofisa Mauzo mwandamizi wa Shirika hilo, Emmanuel Lymo. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,akisiliza maelezo kuhusu matumizi ya Nyaya za Africab kutoka kwa Ofisa Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Khuzema Janowalla, wakati Makamu alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho ya kwanza ya Tanzania Homes Expro, yaliyofanyika leo Juni 10 katika Viwanja vya Mlimani City Mwenge jijini Dar es Salaam.(Picha na Muhidin Sufiani-OMR).

No comments:

Post a Comment