Shirikisho la Ngumi la Kimataifa na Chama Cha Ngumi Cha Marekani (IBF/USBA) limeanzisha programu ya kila mwaka ya kupanda mlima Kilimanjaro ili kuutangaza utalii wa Tanzania kote ulimwenguni.
Programu hiii inayofahamika kama “IBF Mount Kilimanjaro Climb Expedition” itawashirikisha manachama wote wa IBF/USBA, familia zao, marafiki na wapenzi wa IBF/USBA na ngumi kote ulimwenguni.
Akiwakilisha Mradi wa “IBF Sorts Tourism” katika mkutano wa 29 wa shirikisho hilo uliofanyika katika jiji la Honolulu, jimbo la Hawaii nchini Marekani, Rais wa IBF/USBA katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi alitaja kuwa programu hiyo itaanza rasmi mwezi wa December mwaka huu.
“IBF/USBA Mount Kilimanjaro Climb Expedition” itakuwa moja kati ya program zilizopo katika Mradi wa “IBF Sports Toirism” ambao lengo lake ni kuitangaza Afrika kama sehemu muafaka ya kutembelea na kuwekeza. Programu hii inaanzia katika nchi za Ghana na Tanzania kama nchi mbili za Afrika zilizoteuliwa (Pilot Countries).Tanzania itafaidika na mtandao mpana wa IBF/USBA ambao uko katika nchi zaidi ya 204 duniani.
Kuanzishwa kwa programu hii ya “IBF/USBA Sports Tourism” pamoja na programu tanzu ya “IBF Mount Kilimanjaro Climb Expedition” kutaifanya Tanzania kufaidika na ujio wa watalii wengi kutoka katika mataifa makubwa kama Marekani, Canada, Brazil, Ujerumani, Uingereza, Italia, Ufaransa, Urusi, China, Japan pamoja na chi za Scandinavia. Watalii toka mataifa haya wanajulikana kwa matumizi yao makubwa ya fedha.
Tunawahamasisha Watanzania wajihusishe sana na Mradi huu ili waweze kufaidika na bishara zitakazojitokeza. Wenzao wa Ghana kwa sasa wanawasiliana na wahusika wa Mradi huu ili kuitumia vizuri kwa faida yao na Nchi yao. Sio vizuri Watanzania wakawa watu wa mwisho kwa kila jambo.
No comments:
Post a Comment