Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-Moon (Pichani) amefungua rasmi mkutano wa siku tatu wa maendeleo endelevu nchini Brazil huku akionya kuwa muda hautungoji kwa kuweka sawa orodha ndefu ya matatizo ya mazingira.
Nchi wanachama 191 wa Umoja wa Mataifa ikiwa ni pamoja na marais 86 na viongozi wa nchi wanahudhuria mkutano huo wa Rio.
Mkutano huo unafanyika miaka 20 baada ya mkutano wa kwanza wa dunia, wakati mataifa yalipoahidi kurejesha nyuma mabadiliko ya tabia nchi, kuenea kwa jangwa na kutoweka kwa baadhi ya aina za viumbe.
No comments:
Post a Comment