Tume ya uchaguzi ya Libya imeahirisha uchaguzi wa bunge nchini humo hadi tarehe 7 mwezi Julai mwaka huu kwa sababu zilizoitwa za uratibu.
Uchaguzi huo ulipangwa kufanyika tarehe 19 mwezi huu lakini Mkuu wa tume ya uchaguzi Nuri al Abbar (pichani) amesema kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kutatoa muda zaidi kwa wapigaji kura kujisajili na rufaa za watu waliokatazwa kugombea zishughulikiwe.
Uchaguzi huo utakuwa wa kwanza wa kitaifa baada ya miongo minne ya utawala wa aliyekuwa kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gadhafi, ambaye aliuwawa na waasi mwezi Oktoba mwaka jana.
Hadi kufikia wakati huu wananchi milioni 2.7 wa Libya wamejiandikisha kupiga kura.
No comments:
Post a Comment