Serikali ya Tanzanzia kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo imesema kuwa hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji matokeo , ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la ‘Islamic Knowledge’ zilizokokotolewa na Mfumo wa kompyuta zilikuwa na tofauti.
Akizungumza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Mh. Shukuru Kawambwa amesema amesema alama hizo zilitofautiana na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi.
Mh. Kawambwa amefafanua kuwa uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo kwenye mfumo wa kompyuta ulionesha kuwa uchakachaji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya “paper” tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment