Tuesday, June 12, 2012

Tanzania Journalists Alliance (TAJOA)

Shinda muda wa maongezi Sh. 20, 000

Mara nyingi wananchi wamekuwa wakikaa pembeni na kulalamika nchi inapokumbwa na dhahma na kuwarushia mzigo viongozi na watendaji wengine. Kulalamika imekuwa tabia ya Mtanzania.
Sasa muda umefika kwa kila mmoja kuwa sehemu ya kupatikana kwa ufumbuzi wa matatizo yetu.

Tajoa, kwa kuanzia imeamua kutoa muda wa maongezi (wa Sh. 20, 000 kwa simu za mkononi kwa mtandao wowote), kwa mtu ambaye ataandika makala (posti) fupi nzuri ya kusaidia kupatikana kwa ufumbuzi wa matatizo ya ukosefu wa madawati, majengo, walimu bora na vifaa vingine vya kufundishia.

Makala hayo yatachapishwa kwenye magazeti ya kitaifa na kwenye blogu zinazotembelewa na idadi kubwa ya watu ili ‘wakubwa’ wetu wasome na kuona kama wanaweza kuchukua mawazo yako.
Karibuni wote. Kila mmoja, bila kujali umri, jinsi wala kiwango chake cha elimu anaruhusiwa kushiriki.

Wananchi ndiyo watakuwa waamuzi, kwa ku-like makala ambayo wataona inafaa. Makala yenye like nyingi ndiyo itashinda.

Mwisho wa kutuma makala hayo ni Juni 20 na matokeo yake yatatangazwa Juni 22, 2012.

No comments:

Post a Comment