Saturday, June 16, 2012

TWIGA STARS FUNGA ETHIOPIA LEO

TIMU ya soka ya Wanawake "twiga Stars' leo itashuka katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam kukwaana na wenzao Ethiopia katika mechi hiyo ya marudiano kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Nane za Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu nchini Equatorial Guinea.
Mshindi baada ya matokeo ya mechi ya awali ambapo Twiga Stars ilifungwa mabao 2-1 na mechi ya Jumamosi atafuzu kwa fainali hizo za Equatorial Guinea.  Nchi ambazo tayari zimefuzu kwa fainali hizo ni wenyeji Equatorial Guinea na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC).
 DRC ilikuwa icheze raundi ya pili na Equatorial Guinea, lakini baada ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuipa uenyeji Equatorial Guinea, DRC nayo imefuzu moja kwa moja kucheza hatua hiyo ya fainali.
Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 10,000 kwa VIP A na sh. 5,000 kwa VIP B na C. Sehemu nyingine zilizobaki kiingilio ni sh. 2,000 na tiketi zitauzwa uwanjani siku ya mechi kuanzia saa 3 asubuhi.

picha na Globalpublisherstz.

No comments:

Post a Comment