Sunday, July 1, 2012

ZAWADI ZAMWAGWA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA


NA MWANDISHI WETU
BAADHI ya madereva wa daladala wanaofanya safari  kati ya Hospitali ya Taifa Muhimbili na maneo mengine jijini  Dar es Salaam, wamesema hesabu ya makusanyo yao imeshuka tangu kuanza kwa mgomo wa madaktari.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti nafullshangweblog.comjijini leo, walisema hali hiyo ikiendelea kwa zaidi ya mwezi kunauwezekano wakuomba kubadilishiwa njia.
Walisema kushuka kwa mapato kunatokana na baadhi ya wanachi waliyokuwa wakienda kupata matibabu, wengine kwenda kusalimia wagonjwa au kufanyabiashara kusitisha kwenda huko.
Mmoja wa madereva hao Hamisi Kato ambaye gari lake linafanya safari zake kati ya Vingunguti na Muhimbili alisema tangu kuanza kwa mgomo huo wamekuwa wakifanya kazi ya hasara.
Alibainisha kuwa kile wanachokusanya kwa siku hakitoshi kugawana na mmiliki ambapo matokeo yake wamekuwa kama wakiwafanyia kazi wamiliki hao.
George Charles, kondaktari wa daladala kutoka Mbezi hadi Mhuhimbili alisema hivi sasa matumaini yao katika makusanyo  yanatokana na abiria wanaosafiri kati ya Mbezi hadi Faya.
Hata hivyo hakuwa tayari kutoa ufafanunuzi wa makusanyo ya wali na ya sasa kwa madai kuwa hiyo ni siri yake.
Aidha, Charles alisema si kitu cha kawaida kwa gari kutoka hospitalini hapo huku likiwa na nafasi wazi kitendo ambacho kwa sasa kimekuwa cha kawaida tangu mgomo huo ulipoanza.

CHANZO NA FULLSHANGWE BLOG

No comments:

Post a Comment