Saturday, January 28, 2012

MSD YAIpiga jeki TWIGA STARS SH.MIL 10 jijini dar leo.

Mkurugenzi wa Shughuli za Kanda za Mashariki wa Bohari ya Dawa (MSD), Lucy Nderimo (kushoto) akimkabidhi Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah hundi yenye thamani ya sh. mil. 10 ikiwa ni msaada kwa timu ya Taifa ya Soka ya Wanawake ya Twiga Stars, katika hafla iliyofanyika Dar es Salaam leo. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Meneja wa Huduma kwa Wateja na Uhusiano wa MSD, Salome Mallamia. Timu hiyo inapambana na Namibia kesho katika mechi ya marudiano ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wanawake.

No comments:

Post a Comment