Wapendwa ndugu mawakala wa Mpesa,ningependa kuwa taadharisha na matapeli ambao wamekuwa wengi sasa,
Sasa kuna jamaa ambaye ameweza kufanikiwa kuvamia mawakala kadhaa ndani ya jiji la Dar es salaam kwa kasi ya ajabu kijana uyu amekuwa akitembelea pikipiki akiwa na kijana mwingine
Wakiwa pamoja naye huwa wanatembea wote,yeye akiwa amesha soma ramani nzima ya eneo lako la biashara na akijua huwa anakuja kamili, bastola na kukuvamia
Lakini baada ya watu kujua kwa muda mrefu,kwasasa amebadili aina ya usafiri anatembelea gari na wapo wawili katika hilo gari yao.
Kisa kingine kilicho tokea Tandika katika hali ya kuvamia mawakala hawa sasa imekuja staili nyingine wakishajua eneo ulilipo kama usalama wa biashara yako yanii kama huna mlizi wakuleweka wao huja usiku maara baada ya kufunga duka wao hutoboa paa la nyumba na kuingia ndani na kusomba pesa zote na mali zote watakazo zikuta.
Wapendwa naomba kueni makini na wateja ambao hujawai kuwaona na hasa wale wanaokuwa wanajifanya wajuwaji tafadhali wafukuzeni kunusuru usalama wa biashara yako.
Mimi dau
Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment