Monday, April 30, 2012

AMANI YATOWEKA MIONONI MWA WAKRISTO NCHINI KENYA NA NIGERIA KUTOKANA NA MASHAMBULIZI.

Watu zaidi ya 15 wameuawa baada ya kushambuliwa  kwa mabomu na bunduki walipokuwa katika ibada kwenye chuo kikuu katika mji wa Kano kaskazini mwa Nigeria.
Msemaji wa Polisi wa jimbo la Kano amearifu kuwa polisi inawasaka washambuliaji wanaoaminika kuwa  bado wapo karibu na sehemu hiyo ya chuo kikuu cha Bayero kinachohusiana na madhehebu ya kikatoliki.
Mashuhuda wamesema watu kadhaa wamejeruhiwa lakini haijajulikana iwapo washambuliaji wa kujitoa mhanga walihusika.
Mpaka sasa hakuna aliesema kuwa alihusika na mashambulio hayo lakini mashambulio ya  aina hiyo yaliyofanyika katika siku zilizopita nchini  Nigeria yalifanywa na kundi la waislamu wenye itikadi kaliwa kundi la Boko Haram. 


No comments:

Post a Comment