Monday, April 30, 2012

MAN CITY Vs MAN UNITED LEO NI KAMA FAINALI NA SIO VITA ASEMA ‘ROBERTO MANCINI’.

Manchester City leo wanatarajiwa kuwa wenyeji wa wapinzani wao wa muda mrefu kutoka mji mmoja, Manchester United, huku Man City ikijua wazi ushindi wowote utawapa nafasi ya kushikilia uskani wa ligi kuu ya Uingereza na uwezekano wa kutwaa taji la ligi hiyo maarufu duniani.
Man United inaenda uwanja wa Etihad ikiongoza ligi kwa pointi 3 zaidi ya Man City ila ikiwa nyuma kwa idadi ya magoli, sababu inayotoa matumaini kwa Man City kuongoza ligi iwapo itashinda mechi ya leo.
Wiki iliyopita Man City ilifanikiwa kuifunga Wolves bao 2-0 wakati Man United ikilazimishwa sare ya 4-4 dhidi ya Everton.
Mara ya mwisho kukutana katika mechi ya Ligi City waliizamisha United kwenye uwanja wa OldTrafford kwa goli 6-1, ikiwa ni uwanja wa nyumbani Man United haikuwaikufungwa idadi hiyo kubwa ya magoli nyumbani tangu mwaka 1930.
Akizungumzia mechi hiyo Sir Alex Ferguson amesema mchezo huo ni muhimu sana kwao hasa kwa mashabiki wao kutokana na upinzani wa miaka mingi uliopo dhidi ya mahasimu wao. Kocha wa Man city Roberto Mancini amekili kuwa itakuwa ni mechi ngumu kwao sababu United si timu ndogo, lakini pia amesisitiza kuwa hiyo ni mechi tu ya football na sio vita.


No comments:

Post a Comment