Msimamizi wa mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi, Jackob Kambili kutoka UTPC Mwanza akisisitiza jambo wakati wa mafunzo.
Baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Singida waliohudhuria mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Mwezeshaji wa mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Singida, Nyaronyo Kicheere akitumia ramani ya dunia katika kutoa mafunzo.
Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Singida wakifuatilia kwa makini mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyokuwa yakitolewa na mwezeshaji Nyaronyo Kicheere (hayupo kwenye picha) .
Na.Nathaniel Limu
Klabu ya waandishi wa habari (SINGPRESS) mkoani Singida kwa kushirikiana na Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPG), kimeandaa mafunzo ya siku sita ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa wanachama wake 10.
Mafunzo hayo yanafanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa Katoliki mjini Singida.
Mwezashaji wa mafunzo hayo ni wakili wa kujitegemea Nyaronyo Kicheere na yanasimamiwa na Jackob Kambili kutoka UTPC, jijini Mwanza.
Akitoa mada zake, Nyaronyo aliwataka waandishi wa habari kwanza kuhakikisha wanakuwa na taarifa za uhakika na zilizojaa ukweli mtupu kabla hawajaandika habari za uchunguzi.
“Jihadharini sana na taarifa za uvumi, msifanyie kazi mambo ya uvumi, hakikisheni mnafanyia kazi taarifa zenye sifa, taarifa zinazoweza kuthibitishwa endapo itahitajika”,alifafanua Nyaronyo.
Aidha, aliwataka kufanya juhudi zaidi katika kutafiti taarifa za uchungi ili ziweze kukidhi mahitaji.
”Mkifanya hivyo,habari mtakazozitoa zitaonyesha umahiri na uwezo wenu na kwa njia hiyo,mtakuwa mnajijengea heshima mbele ya jamii”, alisema.
No comments:
Post a Comment