Kwa mujibu wa mwandishi wa MO BLOG aliyepo eneo la tukio (Viwanja vya Leaders) ambako mwili wa marehemu Steven Kanumba uliwasili majira ya saa tatu kwa ajili ya misa na kuagwa.
Zoezi la kuaga limeshindikana kwa upande wa umati mkubwa wa wananchi waliohudhuria hapo baada ya viongozi pekee kupata fursa ya kuaga na kufuatiwa fujo na polisi kushindwa kudhibiti kulingana na idadi kubwa ya waombolezaji.
Hivyo mwili wa msanii huyo maarufu wa filamu unaelekea kuzikwa katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam huku gari iliyobeba mwili wake ikisukumwa na wananchi waliojipanga barabarani kuelekea makaburini.
No comments:
Post a Comment