Monday, April 23, 2012

Kwa msimamo wa Ligi kuu inaonesha Simba Ni Kama Bingwa ni baada ya kuifunga Moro magoli matatu kwa bila

Mashabiki wa timu ya Simba wakishangilia kwa furaha mara baada ya timu yao kufanya vizuri na katika mchezo wao na timu ya Moro United.
Picha kwa hisani ya Full Shangwe Blog

 Mchezaji wa timu ya Moro United Eric Mawala akijaribu kuokoa mpira, huku mchezaji wa Simba Emmanuel Okwi akimkaba katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliofanyika kwenye uwanja wa taifa jioni hii jijini Dar es salaam, ambapo Simba imeibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya timu ya Moro United, kwa matokeo hayo Simba imefikisha pointi 59.

Magoli ya Simba yamefungwa na wachezaji Haruna Moshi, Patrick Mafisanga pamoja na Mchezaji Felix Sunzu kutoka nchini Zambia.


Shabiki wa simba akiwa amepagawa kwa ushindi




Full Time Simba 3 -  Moro 0,
na huko Chamazi Azam 1 - Mtibwa 1
 kwa Matokeo hayo Simba ni kama mabingwa wa Ligi kuu kulingana na msimamo wa ligi ulivyo mpaka sasa
Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog

Kikosi cha timu ya Simba

No comments:

Post a Comment