Monday, April 23, 2012

SERGIO AGUERO NA SAMIR NASRI WAREJESHA MATUMAINI YA UBINGWA MAN CITY, WOLVE YASHUKA DARAJA RASMI IKIWA BADO NA MICHEZO MITATU.

Sergio Aguero na Samir Nasri wamefanikiwa kufufua ndoto za ubingwa ligi kuu Uingereza  kwa Man City katika  mechi ya jana tarehe 22/04/1212, magoli mawili (2) walofunga  ugenini ndo ulozamisha jahazi la wenyeji wao Wolverhamton Wanderers na kupoteza rasmi nafasi ya kucheza Premier League Msimu ujao.
Manchester City imefanikiwa kupunguza utofauti wa point huku ikiwa na idadi nzuri ya magoli dhidi ya kinara wa ligi hiyo sasa  Manchester United  , kwasasa Manchester United inaogoza ligi ikiwa na point 83 baada ya kucheza michezo 35 sawa na Manchester City  wenye point 80.
Mahasimu hawa kutoka mji mmoja (Manchester) wanatarajia kuumana katika mchezo wao wa marudiano tarehe 30/04/2012 katika uwanja wa Etihad mchezo ambao kwa kiasi kikubwa utaamua ni nani kuwa bingwa wa ligi kuu nchini Uingereza.


No comments:

Post a Comment