Serikali ya Waziri Mkuu Mark Rutte (Pichani) wa Uholanzi imejiuzulu baada ya mazungumzo kuhusu hatua za kubana matumizi kutofikia muafaka.
Rutte aliwasilisha barua ya kujiuzulu kwa Malkia Beatrix katika makao yake mjini The Hague.
Serikali ya muungano inayoongozwa na Rutte yenye siasa za wastani za mrengo wa kulia, ilishindwa kuafikiana na chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Freedom Party, kuhusu mpango wa kupunguza kwa asilimia kubwa gharama za matumizi ya bajeti ya serikali baada ya wiki kadhaa za mazungumzo.
Hatua hiyo ya kujiuzulu sasa inaweka nafasi ya kufanyika kwa uchaguzi wa bunge.
No comments:
Post a Comment