Rais Mwai Kibaki (pichani) wa Kenya leo analihutubia taifa ambapo anatarajiwa kulitaka bunge kuharakisha kupitisha mswada wa sheria ya mabadiliko.
Rais huyo atatoa hotuba hiyo muhimu kuzungumzia hali ya umoja wa kitaifa nchini humo akiwa katika kiti cha spika wa bunge, katika ukumbi wa zamani wa bunge, kipindi hiki ambacho nchi hiyo iko katika hali ya mkanganyiko na huku baadhi ya washirika wake wakuu wakikabiliwa na mashitaka katika Mahaka ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC).
Kitendo cha kuhutubia akiwa katika kiti cha spika wa bunge kinamaanisha kuwa hotuba yake haitajadiliwa pindi atakapomaliza kuhutubia.
Badala yake hotuba hiyo itwasilishwa baadae na Makamu wa Rais Bw. Kalonzo Musyoka ambaye ndie kiongozi wa shughuli za serikali bungeni.
Kalonzo atawasilisha hoja ya kuijadili hotuba hiyo kwa siku 4 za vikao vya bunge.
No comments:
Post a Comment