Dr. Badru Kiggundu (Pichani) bosi wa tume ya uchaguzi Uganda na wafanyakazi wa tume hiyo wamedai ongezeko la mshahara ili kuweza kufanya kazi zao kwa ufanisi nakujituma, ili kutimiza hitaji kubwa katika katiba la uchaguzi huru na wa haki.
Kwasasa Dr. Kiggundu analipwa kiasi cha shg milioni 5 pesa ya Uganda, amesema mshahara huo ni mdogo na hicho ndo chanzo cha baadhi ya watendaji kuachia ngazi katika tume hiyo.
Akizungumza na vyombo vya habari Bosi huyo amesema tangu mshahara upangwe mwaka 1999 haujawahi kuongezwa wakati gharama za maisha zimepanda kwa kiasi kikubwa. Dr. Kiggundu amesema “ wafanyakazi wa mmlaka ya mjini mkuu Kampala wanalipwa na serikali mshahara mkubwa unaokidhi hali ya sasa ya uchumi nchini Uganda, kwanini isiwe na sisi?”
“Tumekuwa kama yatima” alisema Dr. Kiggundu japo alikataa kuweka wazi ni kiasi gani cha pmshahara angehitaji kulipwa na Serikali ya Uganda.
No comments:
Post a Comment