Thursday, May 3, 2012

MOURINHO AREJESHA KOMBE LA – LA LIGA MADRID.

Jose Mourinho jana amefanikiwa kurejesha kombe la La Liga kwa kilabu cha Madrid , ikiwa ni msimu wa pili tangu aanze kuinoa timu hiyo.
Ikiwa ni siku chache tu tangu kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kutangaza kuachia ngazi kwenye timu hiyo Barca wamekuwa  wapinzani wa Real Madrid wa muda mrefu na kila wanapocheza mechi yoa utazamwa kama fainali.
Guardiola akiiongoza Barca amefanikiwa kutwaa vikombe 13. Kwa upande wa Mourinho msimu wa kwanza haukwenda vizuri na kuonekana kama anapoteza muelekeo, baada ya kutwaa kombe la Mfalme pekee, huku akifungwa na Barca mara nyingi  kitu kilichowapa wasiwasi mashabiki wa Madrid.
Rais wa timu ya Real Madrid, Florentino Perez alimleta Mourinho kuinoa timu yake mwaka 2010 akiwa na matarajio makubwa ya kupata vikombe vingi baada yakocha huyo kupata mafanikio na timu za Porto, Chelsea na Inter Milan.



No comments:

Post a Comment