Thursday, May 17, 2012

CCM YATAKA MISINGI MIKUU YA TAIFA KUBAKI KATIKA KATIBA MPYA.

Na.MO BLOG TEAM
Halmashauri kuu ya CCM Taifa imekubaliana kuwa wanachama na wananchi kwa ujumla wahakikishe kuwa misingi mikuu ya taifa letu inabaki katika katiba mpya itakayoandikwa.
Akizungumza na vyombo vya habari leo jijini Dar es Saalam, Katibu wa halmashauri Kuu ya taifa ya CCM anayeshughulikia Itikadi na Uenezi Nape Moses Nnauye (pichani) amesema misingi hiyo ni pamoja na Kuwapo kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kendelea kuwapo kwa mihimili mitatu ta Dola ambayo ni Serikali, Bunge na Mahakama.
Amesema misingi mingine ni kuendelea kuwapo kwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na pia kuendelea kuwapo kwa Umoja wa Kitaifa, Amani, Utulivu, Usawa na Haki.
Katika taarifa aliyoitoa kwa waandishi wa habari amesema sheria inayosimamia mchakato wa mabadiliko ya katiba nchini imevipa uhuru vyama vya siasa kushiriki kwenye mchakato wa mabadiliko ya katiba.
Hivyo wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha Mapinduzi wakiongozwa na Mwenyekiti wake Dkt. Jakaya Kikwete walifanya semina mnamo Mei 13 mwaka huu kuhu mwongozo wa CCM katika kushiriki mjadala wa katiba mpya.
Nape amefafanua kuwa katika semina hiyo wajumbe wa halmashauri kuu ya taifa walijadili maeneo ya Misingi Mikuu ya Taifa ambayo yanatakiwa kubaki ndani ya katiba mpya; na Mambo ambayo hayagusi Misingi Mikuu ya Taifa lakini ni muhimu kwa nchi, mambo ambayo yako wazi kwa mjadala mpana.


No comments:

Post a Comment