Thursday, May 17, 2012

WAWAKILISHI WA TANZANIA BIG BROTHER STARGAME 2012 WASEMA WAKO TAYARI KUTUMIKA KATIKA KAZI ZA KIJAMII.

Pichani Juu na Chini ni Afisa Mahusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi (kushoto) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam ambapo ametolea ufafanuzi mfumo uliotumika mwaka huu katika kuchagua nchi itakayotoka katika shindano hilo ambao ni tofauti na miaka mingine.
Amesema washiriki wetu sasa wamerudi nyumbani na tukubali kuwa ‘Asiyekubali kushindwa si mshindani’ hivyo tuwape ushirikiano japo hawakushinda lakini wametuwakilisha vyema.

Aliyekuwa Mwakilishi wa Tanzania katika Shindano la msimu wa 7 wa  Big Brother Stargame 2012 Julio Batalia akielezea furaha yake alipokutana na washiriki wa nchi zingine na jinsi alivyosikitishwa na kitendo cha kuaga shindano hilo mapema, hata hivyo ameelezea kufurahishwa na “Seiduu” kutoka Angola ambaye kwa kukutana naye imesaidia kuitangaza Tanzania kwa kuwa amekuwa akijiita sharobaro wa Tanzania.
Mshiriki wa Big Brother Stargame 2012 Hilda Reiffenstein amefafanua ukaribu wake na mshiriki mwenzie Julio kuwa ni marafiki wa siku nyingi na sio kama watu wanavyofikiria, ambapo pia amezungumzia matarajio waliyokuwa nayo katika shindano la mwaka huu tofauti na matokeo yalivyokuwa. Hilda pia ameeleza utayari wao kushiriki katika maswala yote ya kijamii hapa nchini na kuwataka wadau wasisite kuwatumia.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Multichoice Tanzania Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo ambapo amewataka wateja wote wa DStv wasivunjike moyo kuona Watanzania wametolewa na kuwasihi kuendelea kutazama shindano  Big Brother Stargame 2012 na kushiriki katika kupiga kura kwa mshiriki watakayempenda
Baadhi ya Watangazaji na waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.

Mtangazaji wa televisheni ya  Channel Ten Salma Msangi a.k.a Kimora Lee wa Bongo katika snap ya Ukumbusho na Washirikiwa shindano la Big Brother Stargame 2012 waliorejea nyumbani jana baada ya kutolewa katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment