Kocha Kenny Dalgish wa Liverpool (Pichani) ametamba kuiongoza timu yake kwa kujiamini kwenye fainali za FA Cup dhidi ya Chelsea kwenye uwanja wa Wembley. Dalgish amesema kipigo walichopata nyumbani kutoka kwa Fulham cha goli 1-0 kwa jinsi yoyote hakina athari kwenye mudi na hari walionayo kwaajili ya mchezo wa fainali ya FA.
Dalgish amekiri udhaifu wake na amekubali kubeba lawama za kufungwa kwao huku akisema aliamua kuwapa wachezaji wengine pia fursa ya kuingia uwanjani baada ya kukaa benchi mara nyingi.
Pamoja na kufungwa Dalgish amemsifia Mchezaji Andy Carroll akisema ameonesha uwezo mkubwa kwenye mechi hiyo na hivyo kujiongezea uwezekano wa kucheza fainali za FA.
No comments:
Post a Comment