Friday, May 25, 2012

DKT. BILAL KATIKA MKUTANO WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA MJINI BOTSWANA.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Mama Asha Bilal, wakiingia kwenye ukumbi wa tafrija ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana Lt General Seretse Khama kwa viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika Nchini Gaborone Botswana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal kushoto, Rais wa Liberia Mhe. Ellen Jonson na Rais wa Botswana Mhe. Lt General Seretse Khama wakiwa kwenye tafrija ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Rais wa Botswana kwa Viongozi wakuu wa Afrika waliohudhuria mkutano wa siku mbili kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika jana jioni.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal wakiwa kwenye tafrija iliyoandaliwa na Rais wa Botswana Lt. General Seretse Khama kwa ajili ya viongozi wakuu wa Nchi za Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu maendeleo endelevu kwa Bara la Afrika.
Wasanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni nchini Botswana wakitumbuiza kwenye mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu maendeleo endelevu ya Bara la Afrika unaoendelea leo mjini Gaborone Botswana.(Picha na VPO).

No comments:

Post a Comment