Friday, May 25, 2012

VODACOM YAZINDUA PROMOSHENI YA WIKIENDI YA WAJANJA.


-Wateja wa Vodacom kupata nyongeza ya  asilimia 50 kila wanapoongeza muda wa maongezi kuanzia  Tsh 1000
-Nyongeza hii inaweza kutumika kwa ajili ya  a kutuma ujumbe mfupi SMS, kupiga simu au kuperuzi internet.
-Kujua Salio la nyongeza mteja anaweza kubonyeza *102*02#
Kampuni ya mawasiliano inayoongoza Tanzania, Vodacom leo imezindua promosheni kwa ajili ya wateja wake ambapo kuanzia leo hadi mwisho wa wikiendi watapata nyongeza ya asilimia hamsini kila mara wanapoongeza muda wa maongezi wa kuanzia Tsh1000.
Katika taarifa kwenye vyombo vya habari, Mkurugenzi Mtendaji  wa Vodacom Tanzania Bw. Rene Meza alisema promosheni hii imetokana na kuguswa kwa wateja na kampeni iliyozinduliwa hivi karibuni ya WAJANJA ambayo imeonyesha kupendwa na kutumiwa sana na wateja wao kwenye matumizi ya kupiga simu, kutuma ujumbe mfupi SMS na kuperuzi kwenye internet.
“Tunajivunia tunapowaona wateja wetu wakifurahi na kuendelea kutumia huduma zetu na hii promosheni inanuia kuwapa thamani zaidi yapesa zao wakati huu wa wikiendi ikiwa ni fursa kubwa kwa familia kufanya shughuli kadha wa kadha,” alisema Bwana Meza.
Nyongeza hii ya salio ya asilimia 50 inaweza kutumika kwa kutuma ujumbe mfupi, kupiga simu na kuperuzi internet kupitia simu za mkononi na pia promosheni hii ni kwa ajili ya  wateja wanaotumia Mpesa kununua muda wa maongezi.
Wateja pia wanaweza kuangalia salio la nyongeza hii kwa kubonyeza *102*02#

No comments:

Post a Comment