Thursday, May 24, 2012

EMAMANUEL TAGOE AVULIWA UBINGWA WA IBF.


Shirikisho la Ngumi la Kitaifa bara la Afrika, mashariki ya kati na Ghuba ya Uajemi (IBF) limetangaza kumvua ubingwa wa mabara katika uzito wa Junior Light uliokuwa unashikiliwa na bondia Emmanuel Tagoe wa Ghana (Pichani).
Katika kumvua ubingwa huo ambao Tagoe alikuwa autetee tarehe 26 May Rais wa Shirikisho hilo barani Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi bwana Onesmo Ngowi alisema kuwa Tagoe anavuliwa ubingwa kutokana na kudanganya kwake kwenye vipimo vya afya!
Hii ni mara ya kwanza kwa Shirikisho hilo kumvua ubingwa bondia kwa madai ya kudanyanya kwenye vipimo vya afya!
Bondia Emmanuel Tagoe alikuwa azipige na bondia Antonio De Vitis wa Italia kugombea ubingwa wa Junior Lightweight May 26, mwaka huu!
Msimamizi mkuu wa mpambano huo alikuwa Rais wa IBF katika bara la Afrika, Mashariki ya Kati na Ghuba ya Uajemi Mtanzania Onesmo Ngowi. Ngowi pia ni Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania na Mkurugenzi wa Baraza la Ngumi la Jumuiya ya Madola (CBC).
Hii inawaweka mabondia wote katika hali ya hatari ya kuvuliwa ubingwa wao endapo tu wataonekana kuwa wamedanganya katika vipimo vya afya zao. Aidha, tabia ya mabondia wengi kutumia madawa ya kulevya inahatarisha ushiriki wao katika mchezo wa ngumi.
Katika msimamo wake huo Ngowi alisema kuwa ameuchukua uamuzi huo ili kutoa fundisho kwa wale wote wanaofikiri kuwa udannganyifu hususan utumiaji wa madawa ya kuongeza nguvu utawasaidia katika michezo.
Wanamichezo wanatakiwa wajue kuwa vipaji, juhudi za kufanya mazoezi na kujituma ndivyo pekee vitakavyowapa ushindi katika michezo na sio dawa za kulevya.
Matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu yamepigwa marufuku hata michezo mbalimbali kama Olympic, World Cup na mashindano mengi ya ya kitaifa na kimataifa.
Hili ni fundisho rasmi kwa mabondia wa kitanzania wanaotumia madawa ya kulevya kama bangi na mengine ili washinde katika mapambano yao. Kwa kazi hii mchezo utabaki kwa wa wenye vipaji tu!
Imetolewa na
Kitengo cha Mahusiano (PRO)
International Boxing Federation Africa (IBF/AFRICA).

No comments:

Post a Comment