Thursday, May 10, 2012

MH. MEMBE AKANUSHA TUHUMA ZA KUHONGWA PESA NA BAADHI YA NCHI ZA AFRIKA NA KUWA ANAJIANDAA KWA KINYANG’ANYIRO CHA URAIS MWAKA 2015.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (MB), akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Mkutano wa Wizara ya Mambo ya Nje  jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali -Wizarani Bw. Assah Mwambene.
Na.MO BLOG TEAM
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amekanusha madai kuhusiana na kuwa amehongwa pesa na baadhi ya nchi za Afrika ikiwemo Morocco na kuanza kujenga hoteli ikiwa ni mojawapo ya njia za kujiandaa katika kinyanganyiro cha urais mwaka 2015.
Akijibu maswali ya baadhi ya waandishi wa habari waliotaka kujua kuhusu tuhuma zinazomkabili, kama ilivyoripotiwa na chombo kimojawapo cha habari katika mahojiano na mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kitinye, Mh. Membe amemtaka Mzee huyo kutamka wazi jina lake hadharani kuwa yeye ndiye mhusika, ili hatua za kisheria ziweze kufuatwa na kumfananisha mzee huyo kama kingwendu mzee wa majungu.
Katika hatua nyingine Mh. Benard Membe amezungumzia suala la kinyang’anyiro cha Rais wa kamisheni ya Umoja wa Afrika – AU na kusema kuwa nafasi hiyo haijapa mtu mpaka sasa kutokana na mgogoro ulioko baina ya nchi za Magharibi ya Afrika na zile za kusini.
Amesema kuwa hivi sasa Tanzania ikishirikiana na nchi nyingine imependekeza jina la Mama Zuma wa Afrika Kusini na imeamua kumsemea ili achaguliwe kuwa Rais wa kamisheni hiyo katika mkutano wa AU utakaofanyika Lilongwe Malawi Julai mwaka huu.


No comments:

Post a Comment