Wafuasi wa Chama cha CHADEMA wakimpongeza Mh. John Mnyika mara baada ya kuibuka mshindi dhidi ya kesi iliyokuwa ikimkabili.
Mbunge wa Jimbo la Ubungo kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. John Mnyika (wa pili kushoto) akisubiri kusomewa hukumu katika Mahakama Kuu kanda ya Dar es Salaam leo huku akiwa amekaa sambamba na mpinzani wake kwa tiketi ya CCM Bi. Hawa Ng’umbi (wa tatu kushoto).
Pole sana Mama ndio Siasa hiyo” Mmoja wa Wafuasi wa Chama cha Mapinduzi akimpa pole Bi. Hawa Ng’umbi (katikati) mara baada ya kutoka Mahakamani.
Maandamano ya wafuasi wa CHADEMA wakishangilia ushindi wa Mbunge John Mnyika wakielekea katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho.
Mh. John Mnyika ameshinda kesi ya kupinga ushindi wake katika Jimbo la Ubungo katika hukumu iliyotolewa leo na mahakama kuu ya Tanzania na kukifanya chama cha CHADEMA kuendelea kushikilia jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment