Familia pamoja na mamia ya marafiki wa aliyekuwa ‘Malikia wa Disco’ Donna Summe wamehudhuria mazishi yaliyofanyika kwa faragha huko Nashville katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.
Katika mazishi hayo kamera hazikuruhusiwa katika ibada iliyofanyika katika kanisa la Christ Presbyterian lililoko katika jiji hilo, ambako mwanamuziki huyo mshindi mara tano ya tuzo ya Grammy alikuwa akiishi tangu mwaka 1995.
Wageni waalikwa walikuwa ni pamoja na mtayarishaji muziki na rafiki yake wa karibu David Foster, ambaye aliimba wimbo wa ‘The Prayer’ akishirikiana na muimbaji Natalie Grant.
Mwanamuziki huyo aliyekuwa maarufu kwa jina la ‘Malkia wa Disko’ kutokana na mfululizo wa vibao vyake vilivyovuma, alifariki wiki iliyopita akiwa na umri wa miaka 63 kutokana ugonjwa wa saratani ya mapafu.
fununuhabari: Tutamkumbuka daima kutokana na mchango wake katika tasnia muziki duniani. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi – Amen.
chanzo/source moblog
No comments:
Post a Comment