Thursday, May 17, 2012

PAMOJA NA TUHUMA ZA UBAGUZI WA RANGI JOHN TERRY AREJESHWA KIKOSI CHA ENGLAND, KWAAJILI YA EURO 2012, RIO FERDINAND ATUPWA NJE.

John Terry ni miongoni mwa wachezaji 23 waloitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya uigereza  kwaajili ya michuano ya Euro 2012.
Mchezaji huyo wa Chealse anakabiliwa na shitaka la kumbagua rangi kwa makusudi ndugu wa Rio Ferdinand aitwae Anton.
Rio Ferdinanand ametoswa katika kikosi hicho kama Mashabiki wengi nchini Uingereza walivyotabiri , Rio ambaye amekuwa akicheza kama beki wa kati sambamba na Terry, uamuzi huo wa kocha unamanisha mwisho wake katika michezo ya kimataifa.
Akitetea uamuzi wake kocha Roy Hodgson amesema uteuzi wake umezingatia vigezo tu vya wachezaji na si vinginevyo, kuhusu sakata la Terry kocha amesema kwasasa hatupaswi kumuhukumu hadi mahakama itakapo hakiki hatia dhidi yake.

SOURCE ,NA MOE BLOG

No comments:

Post a Comment