Monday, May 28, 2012

POLISI YAWATAKA WANANCHI ZANZIBAR KUWA WATULIVU.

Polisi katika visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania wamewataka wananchi kuwa watutulivu baada ya kuibuka ghasia zilizosababisha watu kadhaa kujeruhiwa kutokana na maandamano ya kudai uhuru wa visiwa hivyo kutoka Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kamishna wa Polisi visiwani humo Mussa Ali Mussa (Pichani), amesema kuwa vurugu hizo zimesababishwa na maandamano yaliyoitishwa na Jumuiya ya Kiislamu ijulikanayo kama  Uamsho.
Wafuasi wa jumuiya hiyo waliandamana hadi kituo cha polisi kufuatia kukamatwa kwa mmoja wapo wa viongozi wao.
Katika eneo la Mji Mkongwe waandamanaji walirusha mawe huku polisi wakitumia mabomu ya machozi kuwatawanya, huku kukiwa na makundi madogo madogo ya waandamanaji kwenye mji huo.
Jumuiya ya Uamsho inayodai kulinda desturi za Kiislam visiwani Zanzibar imekuwa ikifanya mihadhara kutaka Zanzibar ijitowe kwenye muungano.


No comments:

Post a Comment